Taja sifa zozote tano za maigizo

      

Taja sifa zozote tano za maigizo.

  

Answers


KELVIN
? Hutolewa mbele ya hadhira.
? Uigizaji huhitaji mandhari maalum ya utendaji.
? Hufungamana na shughuli za jamii kama vile mtambaji wa hadithi na sherehe za miviga kama jando, harusi na matanga.
? Sharti kuwe na tendo la kuigiza ambalo lina matendo ya watu na viumbe wengine kwa nia ya kuelimisha, kukashifu, kusifu na kuburudisha.
? Waigizaji wanavaa maleba yanayooana na hali wanayoigiza.
? Maigizo huigiza hali ya maisha ya jamii; kisiasa, kiuchumi na kitamaduni kwa nia ya kuonyesha mafanikio, udhaifu na migogoro katika nyanja za maisha.
? Huwa na muundo mahususi na mtiririko wa matukio tangia mwanzo ukuzaji wa migogoro, kilele na usuluhishaji.
? Maigizo yaweza kuandamana na ngoma, pamoja na uimbaji au ukariri wa tungo za kishairi.

kalvinspartan answered the question on July 24, 2018 at 11:22


Next: Taja vipera vya maigizo vinne
Previous: Maigizo huwa na madhumuni yepi katika jamii

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions