Maigizo huwa na madhumuni yepi katika jamii

      

Maigizo huwa na madhumuni yepi katika jamii

  

Answers


KELVIN
? Huburudisha watazamaji na waigizaji wenyewe. Burudani hii mara nyingine hupumbaza.
? Huhifadhi na kuendeleza utamaduni wa jamii kama vile upashaji tohara, matambiko, majigambo, ngoma, miviga na michezo ya watoto hudumishwa kupitia maigizo.
? Ni kitambulisho cha jamii; kila jamii ina Sanaa ya maigizo ya jamii husika. Miviga na sherehe za arusi na mazishi hutofautiana kutoka jamii moja hadi nyingine.
? Hukuza umoja na ushirikiano wa watu wanapojumuika kushiriki katika maigizo. Hao hujitambulisha kama jamii moja.
? Ni nyenzo za kupitisha maarifa na amali za jamii kupitia michezo ya jukwaani.
? Husawiri mtazamo wa jamii kuhusu masuala mbalimbali kama vile woga, wizi na usaliti.
? Hukuza ubunifu madhalan watoto wanaposhiriki michezo ya watoto, hujifunza kubuni michezo wakiwa wachanga na pia Sanaa ya uigizaji.
? Hukuza kipawa cha uongozi katika michezo, huweza kujifunza stadi za uongozi
? Ni njia ya kuimarisha urafiki. Kwa vile mizaha na utani katika malumbano hukuza urafiki na uhusiano bora
? Huongoza jamii kupambana na na mazingira wanamojipata. Kutegemea imani ya wanajamii,matambiko yanaweza kuondoa matatizo katika jamii kama vile njaa, ugonjwa na ukame kwa kuomba Mungu
? Maigizo huelimisha kupitia maudhui na hulka za waigizaji na kushauri nafsi zao, kuiga au kukashifu hulka hizo.

kalvinspartan answered the question on July 24, 2018 at 11:23


Next: Taja sifa zozote tano za maigizo
Previous: Jadili maana ya malumbano ya utani

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions