Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Malumbano ya utani huchangia umuhimu gani katika jamii

      

Malumbano ya utani huchangia umuhimu gani katika jamii.

  

Answers


KELVIN
a) Hutoa maadili kwa hivyo mila na desturi za jamii huwapa baadhi ya watu katika jamii jukumu la kutaniana na wengine kwa sababu maalum.
b) Malumbano hupunguza urasmi miongoni mwa wanajamii, hivyo huhimiza kujieleza kwa urasmi bila kuficha.
c) Huimarisha urafiki, ni watu walio na uhusiano mwema tu wanaoweza kutaniana.
d) Hukuza utangamano miongoni mwa watu na makabila mbali mbali hasa wanapokuja pamoja kutaniana.
e) Hutambulisha jamii kwa kutaja baadhi ya sifa zake katika utani k.m unaweza kumtania mtu mchoyo, hivyo kumtaka ajirekebishe.
f) Hukosoa na kukashifu tabia hasi baadhi ya malumbano ya utani hudhihaki ulafi, uchoyo, wivu na tabia nyingine mbaya.
g) Huburudisha, ucheshi katika malumbano ya utani huburudisha na kuchangamsha.
h) Huelimisha, kupitia malumbano ya utani, watu hupata maarifa ya kukabiliana na hali mbalimbali maishani.

kalvinspartan answered the question on July 24, 2018 at 11:26


Next: Jadili sifa za malumbano ya utani
Previous: Taja aina mbili za ulumbi

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions