Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Fafanua umuhimu wa ulumbi katika jamii

      

Fafanua umuhimu wa ulumbi katika jamii.

  

Answers


KELVIN
1. Hukuza uwezo wa kujieleza hadharani, kadri mtu anavyozungumza hadharani, ndivyo anavyojiboresha kama mlumbi
2. Ni nyenzo ya kukuza ujuzi na ufasaha wa lugha, jinsi mtu anavyoitumia lugha kwa ugwiji, ndivyo anavyokuza umairi wake wa kuisarifu lugha.
3. Ni msingi wa kuteua viongozi, uwezo wa mtu kuwashawishi wanajamii kukubaliana na mtazamo wake humfanya kutambuliwa kama mwenye uwezo wa kuongoza jamii. Walumbi wana uwezo mkubwa wa kuishawishi hadhira.
4. Huhifadhi utamaduni wa jamii, ulumbi ni sanaa jaadia, imekuwepo katika jamii kwa muda mrefu, ikipokezwa vizazi na vizazi.
5. Ni nyenzo ya kuburudisha wanajamii na kuwaelimisha bila kuwachosha, walumbi huweza kupitisha maarifa mbali mbali kwa wanajamii kwa njia yenye mvuto.
6. Hukuza uzalendo, vijana wanaposikiza walumbi wakitongoa lugha, huionea fahari lugha yao na kujitambulisha zaidi na jamii zao.
7. Huweza kutumiwa kuwasilisha ujumbe muhimu au ulio na athari kubwa au ambao una makali na usio rahisi kueleza.
8. Ni kitambulisho cha utabaka, katika baadhi ya jamiii ulumbi ulihusishwa zaidi na tabaka tawala au watu wenye vyeo vya juu na heshima katika jamii zao. Katika jamii hizi ulumbi ni kigezo cha kuainisha matabaka.
9. Ulumbi ni msingi wa kuheshimiwa katika jamii, walumbi huheshimiwa kwa sababu ya matumizi ya lugha yenye ubingwa na ustadi katika kuyafafanua maswala ya jamii.

kalvinspartan answered the question on July 24, 2018 at 11:31


Next: Taja sifa nne za ulumbi
Previous: Eleza maana ya hotuba huku ukitolea mifano ya hotuba

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions