Hotuba huwa na umuhimu gani?

      

Hotuba huwa na umuhimu gani?

  

Answers


KELVIN
1. Huadilisha na kuasa, hotuba zinazotolewa jandoni au arusi kwa kawaida hunuiwa kutoa nasaha
2. Huelimisha, hotuba za jandoni kwa mfano huwapa vijana maarifa ya kukabiliana na maisha.
3. Huimarisha ukakamavu wa kuzungumza hadharani, kadri watu wanavyotoa hotuba ndivyo wanavyoimarisha umilisi wao wa lugha na ujasiri wa kuzungumza hadharani.
4. Hukuza ufasaha na umilisi wa lugha
5. Hupalilia kipawa cha uongozi, kwa kawaida mahatibu huteuliwa kadri mtu anavyochukua jukumu la kuhutubu katika hafla mbalimbali, ndivyo anavyojitayarisha kuchukua nyadhifa kubwa zaidi za viongozi

kalvinspartan answered the question on July 24, 2018 at 11:35


Next: Eleza sifa tano za hotuba
Previous: Jadili nini maana ya mawaidha

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions