Eleza sifa za mawaidha

      

Eleza sifa za mawaidha.

  

Answers


KELVIN
1. Mawaidha hutolewa katika miktadha mbalimbali; rasmi kama vile jandoni, katika arusi, kwenye maisha darasani na kanisani. Hata hivyo, mawaidha yanaweza kutolewa katika miktadha isiyo rasmi kama vile mzazi anaweza kumpa mwanawe mawaidha nyumbani wakati wa chajio.
2. Katika jamii nyingi, wazee na watu walio na vyeo vikubwa na waliochukuliwa kuwa na hekima ndio waliowapa vijana mawaidha. Hata hivyo, vijana pia wanaweza kutoa mawaidha kwa vijana wenzao wanaohitaji ushauri au pia vijana wanaweza kutoa mawaidha kwa wazee.
3. Hutolewa zaidi kwa wadogo, ambao wanaaminika kuwa wanahitaji kupewa mawaidha maishani. Hata hivyo, yanaweza kutolewa kwa yeyote anayehitaji
4. Mwenye kutoa mawaidha analielewa jambo analowosia kwa undani lazima awe na ujuzi wa kutosha katika mada anayozungumzia.
5. Mwenye kutoa mawaidha hutumia lugha inayoathiri hisia za wanaowosiwa inaweza kuwa na tamathali za usemi kama vile methali.
6. Mawaidha huingiliana na vipera vingine vya fasihi simulizi kama vile methali hufumbata mawaidha pia utambaji ngano, miviga kama vile jando na arusi huandamana na utoaji wa mawaidha aidha yapo mashairi ya waadhi halikadhalika anayetoa mawaidha anaweza kutumia mbazi/vigano ili kusisitiza ushauri anaotoa.
7. Maudhui katika mawaidha ni mapana yaani huweza kugusia maswala kama dini, uongozi, ujasiriamali, elimu na taaluma, unyumba, mahusiano ya kijamii, malezi na afya.

kalvinspartan answered the question on July 24, 2018 at 11:37


Next: Jadili nini maana ya mawaidha
Previous: Eleza sehemu tatu kuu za mawaidha

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions