Eleza sehemu tatu kuu za mawaidha

      

Eleza sehemu tatu kuu za mawaidha.

  

Answers


KELVIN
i) Utangulizi, katika sehemu hii anayetoa mawaidha huanza kwa kauli ya kuvuta makini ya hadhira anaweza kuanza kwa kutoa kiini cha mawaidha, kwa mfano utu uzima huenda na uwajibikaji… baadaye anaelezwa anayofaa kufanya
ii) Uwili, mawaidha huwasilishwa na kusisitizwa kwa kutumia kauli sisitizi na tamathali za usemi kama vile methali, tashbihi, istiara hutumika kuwosia, maonyo na maelekezo hutolewa kutegemea lengo
iii) Hitimisho, mwasilishaji huonyesha msimamo wake kuhusiana na swala analowosia kwa kawaida anayetoa mawaidha huishirikisha hadhira kwa kutaka kujua msimamo au maoni yao kuhusu swala alilowawosia, hadhira inaweza kutaja changamoto zinazohusiana na wosia unaotolewa.

kalvinspartan answered the question on July 24, 2018 at 11:38


Next: Eleza sifa za mawaidha
Previous: Mawaidha yana majukumu gani katika jamii?

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions