Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Mawaidha yana majukumu gani katika jamii?

      

Mawaidha yana majukumu gani katika jamii?

  

Answers


KELVIN
1. Jukumu la mawaidha ni kuelekeza, mawaidha hutoa mwongozo wa jinsi ya kukabiliana na matatizo au jinsi ya kutenda jambo fulani.
2. Huelimisha, mawaidha huwapa wanajamii maarifa ya kuendesha maisha, huwajuza wanajamii kuhusu majukumu ya kijamii na matarajio ya jamiii zao kwao.
3. Huadilisha wanaopewa mawaidha hujifunza maadili kama vile usafi, unyenyekevu, utulivu na kusamehe.
4. Hutambulisha jamii, kila jamii huwa na aina yake ya mawaidha kulingana na thamani zake pia mawaidha hutolewa kwa namna mbalimbali kutegemea jamii.
5. Husaidia kuondoa ujinga katika jamii, huadilisha waliopotoka na kufanya mabaya.
6. Husaidia kuwapa ukakamavu wasio nao na kuwaongezea wengine ujasiri na stadi za kimaisha.
7. Huwaandaa watu kushiriki ipasavyo katika shughuli za kitamaduni, kijamii na kadhalika.

kalvinspartan answered the question on July 24, 2018 at 11:38


Next: Eleza sehemu tatu kuu za mawaidha
Previous: Eleza nini maana ya soga

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions