Ushairi simulizi una sifa zipi?

      

Ushairi simulizi una sifa zipi?

  

Answers


kelvin
1. Ushairi simulizi huwasilishwa kwa njia ya mdomo mbele ya hadhira kwa kukaririwa, kughanwa au kuimbwa. Nyimbo kwa mfano huimbiwa watu hata hivyo, baadhi ya mashairi huimbwa na watu bila kuhusisha hadhira nyimbo za kazi mara nyingi hazina hadhira.
2. Hubuniwa papo hapo na kuwasilishwa kwa hadhira au tungo za awali huwasilishwa kutoka kwa kumbukumbu za mwasilishaji.
3. Tungo za mashari simulizi hutolewa zikiambatana na ala za muziki, uimbaji wa nyimbo huambatana na ala kama njuga na marimba aidha anayejigamba huweza kutumia ala kama vile mkuki anapojigamba.
4. Ushairi simulizi ni sehemu ya utamaduni wa jamii na hupitishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine, nyimbo za jandoni (nyiso) na tendi, kwa mfano hupitishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine.
5. Ushairi simulizi hutumia lugha yenye mvuto mkubwa, yenye mapigo yaliyopangwa kwa muwala na urari.
6. Utungo wa ushairi simulizi huweza kuwasilishwa na mtu mmoja kama ilivyo katika majigambo au kundi la watu kama vile nyimbo nyingi na ngonjera.
7. Ushairi simulizi hubadilika kulingana na anayeuwasilisha, hadhira na wakati.Wimbo mmoja unaweza kuimbwa kwa mahadhi mbalimbali kulingana na mwimbaji, mwasilishaji anaweza kubadilisha wimbo au shairi wakati wa kuimba, kukariri au kughani kutegemea hadhira yake.
8. Hadhira huweza kushiriki katika uwasilishaji wa mashairi simulizi, mwimbaji, kwa mfano, anaweza kuishirikisha hadhira yake katika uimbaji kwa kupiga makofi.
9. Uwasilishaji wa mashairi simulizi, kwa kawaida huandamana na uigizaji. Mwimbaji kwa mfano huambatanisha maneno yake na vitendo kama vile ishara za uso, ishara za mkono, miondoko mbalimbali na upigaji makofi.

kevowmuchiri answered the question on July 24, 2018 at 12:11


Next: Jadili nini maana ya ushairi simulizi
Previous: Ushairi simulizi hufungamana na shughuli au muktadha maalumu mathalani nyimbo hufungamana na shughuli tofauti tofauti.Taja mifano minne

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions