Ushairi simulizi waweza kuiainishwa kutumimia vigezo tofauti. Fafanua baadhi ya vigezo vinavyoweza tumika

      

Ushairi simulizi waweza kuiainishwa kutumimia vigezo tofauti. Fafanua baadhi ya vigezo vinavyoweza tumika.

  

Answers


kelvin
1. Maudhui
a) Mapenzi-hupitisha jumbe za mapenzi.
b) Kutuliza-kuna nyimbo za bembea au bembelezi zinazowatuliza watoto.
c) Kuomboleza-mbolezi huimbwa wakati wa msiba.
d) Kusifu-sifa huimbwa kujisifu mashujaa au waliofaidi umma na kustahili kutambuliwa.
e) Siasa-nyimbo za siasa huwasilisha jumbe za kisiasa.
2. Muktadha au mahali pa uwasilishaji
a) Nyiso-nyimbo za jandoni.
b) Mbolezi-zinazoimbwa kwenye mazishi au kwenye maombolezi.
c) Nyimbo za harusi.
d) Nyimbo za matambikoni ambazo hutolewa wakati wa kutoa kafara au sadaka kwa mizimu, labda baada ya janga.
e) Nyimbo za kazi.
3. Mtindo wa uwasilishaji
a) Maghani hutolewa kwa kalima bila kuimbwa.
b) Nyimbo huwasilishwa kwa mahadhi ya kupanda na kushuka.
c) Shairi utungo unaokaririwa.
d) Tendi au Rara husimuliwa kwa mapigo ya kishairi.
e) Ngonjera huwasilishwa kwa kujibizana.
4. Mwasilishaji
a) Majigambo huwasilishwa na anayejigamba
b) Kwaya uimbaji wa watu wengi

kevowmuchiri answered the question on July 24, 2018 at 12:15


Next: Ushairi simulizi hufungamana na shughuli au muktadha maalumu mathalani nyimbo hufungamana na shughuli tofauti tofauti.Taja mifano minne
Previous: Taja na ueleze baadhi ya umuhimu wa ushairi simulizi

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions