Taja na ueleze baadhi ya umuhimu wa ushairi simulizi

      

Taja na ueleze baadhi ya umuhimu wa ushairi simulizi.

  

Answers


kelvin
Ushairi simulizi hutumiwa kupitisha maarifa au mafunzo ya jamii fulani nyimbo za jandoni, za harusi na dini hutumiwa kupitisha mafunzo maalumu.
b)Ni nyenzo ya kuhifadhi na kupitisha utamaduni na historia ya jamii kutoka kizazi kimoja hadi kingine kwa mfano, tendi zinazosifu mashujaa huendeleza historia ya jamii hiyo kwa kuonyesha matukio kama vile nyimbo za jandoni (nyiso) husawiri utamaduni wa jamii kuhusu jando na kuuhifadhi.
c) Hukashifu tabia hasi kwa nia ya kuhimiza urekebishaji wa tabia hizo nyiso kwa mfano, hukashifu woga, hivyo vijana waoga huhimizwa kujirekebisha. Maghani na nyimbo za kisiasa hukashifu tawala dhalimu.
d) Ni nyenzo kuu ya kukuza umoja na uzalendo miongoni mwa wanajamii kupitia kwa nyimbo zinazosifu mashujaa wa vita, huhimiza vijana kuzionea fahari jamii zao na kujitoa mhanga kuzitumikia aidha wanajamii wanapojumuika pamoja kuimba au kughani katika hafla fulani, hujihisi kuwa kitu kimoja, hivyo uzalendo hujengeka.
e)Ni nyenzo ya kutakakasa hisia kupitia kwa mashairi au nyimbo, watu hutoa hisia za moyoni na kutakaza nyoyo zao mfano mwafaka ni nyimbo na mashairi ya mapenzi ambayo kwayo mtu humtolea mpenzi wake hisia. Rara pia hutumiwa kutekeleza jukumu hili.
f) Huelimisha, hukosoa na kurekebisha jamii nyimbo hutoa maadili ya kuonya na kuelimisha wanajamii nyimbo au mashairi ya sifa, tendi hata mbolezi huonyesha matendo mazuri ya anayeimbiwa na kukashifu wanaoenda kinyume na matakwa ya jamii.
g) Husawiri mfumo wa jamii fulani kisiasa, kiuchumi na kijamii baadhi ya nyimbo huonyesha shughuli za kiuchumi za jamii kama vile ufugaji. Hodiya (nyimbo za kazi) huonyesha shughuli mbalimbali kama vile uwindaji, kilimona uvuvi. Majigambo pia husawiri mifumo ya jamii kisiasa na kijamii.

kevowmuchiri answered the question on July 24, 2018 at 12:16


Next: Ushairi simulizi waweza kuiainishwa kutumimia vigezo tofauti. Fafanua baadhi ya vigezo vinavyoweza tumika
Previous: Fafanua maana ya nyimbo

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions