Orodhesha sifa bayana za nyimbo

      

Orodhesha sifa bayana za nyimbo.

  

Answers


kelvin
a) Sifa bainifu ya nyimbo ni kwamba hutolewa kwa mahadhi ya kupanda na kushuka kwa sauti.
b) Nyimbo hutumia lugha ya mkato yenye mpangilio maalumu wa silabi, mishororo na beti zenye mapigo ya kimuziki.
c) Nyimbo hutumia lugha nzito yenye kuibua taswira na hisia nzito kama za mapenzi, huzuni na furaha.
d) Nyimbo zinapoimbwa, maana nyingi huandamana na ala za muziki kama vile ngoma, baragumu, msewe na zumari.
e) Katika jamii za kiafrika, nyimbo hufungamana na muktadha fulani kuna nyimbo za kazi harusi jando na unyago kuzaliwa kwa mtoto, kumpa mtoto jina, ibada na matambiko.
f) Baadhi ya vifungu katika nyimbo hurudiwarundiwa vifungu hivi huitwa vibwagizo, viitikio au mikarara ya nyimbo.
g) Nyimbo nyingi huandamana na ucheshaji wa viungo kama vile mabega kupiga makofi na mapigo ya miguu.
h) Kimsingi, nyimbo ziliimbwa na makundi ya watu kwa hadhira hai. Hata hivyo, kuna nyimbo zinazoimbwa na mtu mmoja kwa hadhira yake au hata bila hadhira.

kevowmuchiri answered the question on July 24, 2018 at 12:21


Next: Fafanua maana ya nyimbo
Previous: Nyimbo huwa na malengo gani katika jamii?

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions