Nyimbo huwa na malengo gani katika jamii?

      

Nyimbo huwa na malengo gani katika jamii?

  

Answers


kelvin
a) Nyimbo hutambulisha jamii kwa kusawiri shughuli na maisha ya jamii iliyozibuni mathalan nyimbo katika jamii ya wakulima zitasheheni msamiati unaohusu shughuli za kilimo kama vile kuvuna, kupanda na kupalilia.
b) Nyimbo humwezesha binadamu kutakasa hisia zake kupitia kwa nyimbo, binadamu hutoa hisia za moyoni kama vile kujutia kosa alilofanya, mapenzi ama huzuni. Mbolezi humsaidia aliyehathiriwa kutoa hisia za huzuni. Nyimbo za mapenzi kama vile chombezi, humwezesha mpenzi kumfichulia mwenzake hisia za moyoni.
c) Ni mbinu mojawapo ya kuhifadhi na kuendeleza utamaduni wa jamii rekodi za matukio muhimu katika jamii huweza kuhifadhiwa kwa nyimbo na kupitishwa kwa vizazi.
d) Nyimbo hutumbuiza hutumiwa kama burudani, kufurahisha, kustarehesha na kusisimua.
e) Hupitisha amali na mambo ambayo jamii inayothamini, amali hizo hurekodiwa katika nyimbo mbalimbali kama vile za kazi na kurithishwa vizazi vya jamii hiyo. Mawaidha na thamani za jamii hukaririwa katika nyimbo kama nyenzo za kuzirithisha.
f) Nyimbo hutumiwa kuhamasisha watu na kuchochea hisia za kuchangamkia jambo fulani. Nyimbo za kisiasa, kwa mfano huweza kuchochea hisia za kuungana pamoja kutetea haki au kuunga mkono jambo fulani.
g) Nyimbo huakisi ukwasi wa tamaduni za jamii umbuji (ufasaha wa kujieleza) na ujamii (mvuto na uzuri wa kazi ya sanaa) wa jamii hujitokeza katika nyimbo huteuzi wa maneno,ishara na ujumbe katika nyimbo huonyesha ukwasi wa jamii hiyo kifani.
h) Hukuza ubunifu miongoni mwa wanajamii, uimbaji ni kipawa na nyimbo hupalilia kipawa hiki.

kevowmuchiri answered the question on July 24, 2018 at 12:22


Next: Orodhesha sifa bayana za nyimbo
Previous: Eleze sifa nne za bembelezi

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions