Bembelezi huwa na umuhimu gani katika jamii?

      

Bembelezi huwa na umuhimu gani katika jamii?

  

Answers


kelvin
1. Hutumbuiza na kuongoa watoto, bembea hupumbaza na kumfanya mtoto anyamaze au alale anapolia
2. Hutumiwa kama sifa kumsifu mtoto mtulivu, husifu pia somo ya mtoto huyo au wazazi wake.
3. Husawiri mfumo wa kiuchumi wa jamii husika, ikiwa baba ni msasi, mtoto atarajiwa kuwa baba ni msasi jasiri au baba yake yuko karibu kutoka usasini.
4. Huonyesha au kusawiri uhusiano katika jamii kupitia bembea, mlezi huweza kuibua migogoro iliyomo kati yake na wazazi wake au wazazi wa mtoto, hivyo kuonyesha uhusiano kati ya waajiri na wajiriwa.
5. Hutakasa hisia ambazo mwimbaji huweza kuwa nazo
6. Humwelimisha mtoto, hata katika umri huu mchanga, kuhusu mambo na shughuli mbalimbali katika jamii na umuhimu wake au thamani yake katika jamii.
7. Husawiri falsafa au mtazamo wa jamii kuhusu jinsia na matarajio ya jamii kwa jinsia Fulani katika bembea, mlezi anaweza kutaja kuwa machozi ni ya kike iwapo anamtuliza mtoto mwanaume, majukumu ya mtoto wa kiume kwa jamii pia huweza kutajwa mlezi huweza kumtajia mtoto wa kike kuwa anatarajiwa kuwa mlezi mwema.

kevowmuchiri answered the question on July 24, 2018 at 12:25


Next: Eleze sifa nne za bembelezi
Previous: Andika majukumu sita ya nyimbo bembelezi

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions