Eleza maana ya nyimbo mbolezi kisha utolee sifa zake nne

      

Eleza maana ya nyimbo mbolezi kisha utolee sifa zake nne.

  

Answers


kelvin
Hizi ni nyimbo ambazo huimbwa wakati mtu amefariki au wakati wa maafa ama katika halfa za kuadhibisha makumbusho.
Sifa
1. Mbolezi hutofautiana kutoka jamii moja hadi nyingine kutegemea imani ya jamii kuhusu kifo na pia kulingana na aliyekufa.
2. Huimbwa kwa njia ya kuwafariji waliofiwa
3. Husifu aliyekufa kwa kawaida mbolezi hutoa sifa chanya au nzuri za aliyekufa watu mashuhuri katika jamii huweza kutungiwa mbolezi zao mahususi zinazowasifu na kutuja michango yao kwa jamii.
4. Hufungamana na muktadha maalum, mbolezi huimbwa tu katika matanga au wakati wa kuomboleza jambo fulani.
5. Huimbwa kwa toni ya huzuni na pengine uchungu ili kuibua hisia za ndani za mwombolezaji.
6. Huimbwa kwa mwendo wa utaratibu.
7. Huonyesha imani ya jamii husika kuhusu kifo.

kevowmuchiri answered the question on July 24, 2018 at 12:29


Next: Andika majukumu sita ya nyimbo bembelezi
Previous: Mbolezi huwa na majukumu gani katika jamii

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions