Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Nyimbo za kisiasa zinanuwia kutimiza malengo gani?

      

nyimbo za kisiasa zinanuwia kutimiza malengo gani?

  

Answers


kelvin
1. Hukuza umoja wa kisisa miongoni mwa washiriki .wakati wa kupigania uhuru, nyimbo hizi zilitumiwa kama nyenzo za kuwaunganisha watu.
2. Huzindua na kuhamasisha watu, huwapa watu k.m wafanyi kazi, ari ya kupigania haki zao. Nyimbo za kisiasa huwatanabahisha watu kuhusu haki zao na kuwahimiza kupigana dhidi ya unyanyasaji.
3. Husawiri mfumo wa kisiasa na kijamii wa jamii husika na maoni ya wananchi kuhusu mfumo huo. Je, wanaupenda au wanaupinga?
4. Husawiri migogoro iliyopo katika jamii, je ni ya unyanyasaji, uongozi mbaya, unyonyaji, ubinafsi, usawa na uhuru?
5. Hutumiwa kueneza propaganda za kisiasa, baadhi ya nyimbo za kisiasa huimbwa ili kusawiri uzuri wa utawala fulani.k.m KANU yajenga nchi, ni wimbo wa kisiasa ulionuia kuwavutia watu kukipenda chama hiki cha kisiasa.
6. Huimiza uzalendo na mshikamano wa kitaifa, nyimbo za taifa ni mfano wa nyimbo za kisiasa zinazohimiza raia kuionea fahari nchi yake na kuishi kwa undugu.
7. Huweza kutumiwa kama rekodi ya matukio ya kihistoria katika jamii Fulani, baadhi ya nyimbo za kisiasa huzungumzia mapambano dhidi ya ukoloni na historia ya mapambano hayo.
8. Hutumiwa kukashifu uongozi mbaya.
9. Hutumiwa kama sifo kuwasifia viongozi waadilifu na mashujaa wengine wa kisiasa kama vile Harry thuku,Dedan kimathi, Arap moi, Jaramogi Odinga, Kenyatta wa nchini Kenya
10. Huburudisha, hutumbuiza na kustarehesha watu katika shughuli za kisiasa au za kitaifa.

kevowmuchiri answered the question on July 24, 2018 at 12:36


Next: Fafanua maana ya nyimbo za kisiasa huku ukitoa sifa zake tano
Previous: Jadili nyimbo za sifa/sifo

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions