Taja sifa zozote mahususi za nyimbo za sifo

      

Taja sifa zozote mahususi za nyimbo za sifo.

  

Answers


kelvin
1. Sifo husifu na kutukuza watu ambao wamefanya jambo fulani k.m husifu maarusi, waliohitimu jandoni, viongozi wa kisiasa, kiuchumi na kijamii, mbolezi na walioshinda mashindano ya michezo au wa kumiliki kitu, kipawa au hali fulani.
2. Sifo hutumia sitiari kwa usanifu mkubwa, huwalinganisha wanaosifiwa na wanyama ili kuonyesha sifa fulani k.m kiongozi anaweza kufananishwa na simba ili kuonyesha ujasiri
3. Sifo hutumiwa katika miktadha mbalimbali ya kijamii kama vile miviga.
4. Huimbwa kwenye jando kuwasiu mashujaa na kuwapongeza kwa kuingia katika utu uzima
5. Huimbwa kwenye mazishi kama taabili/taabini kuwasifu na kuwakumbusha waliokufa.
6. Huimbwa kwenye arusi kuwasifu maarusi.
7. Huimbwa katika sherehe za kutawazwa kwa viongozi au wafalme.
8. Kuna sifo za kidini zinazomsifu Mungu au mitume kwa mfano kasida ya mzia zinamsifu mtume mohammed.
9. Sifo pia huweza kuimbwa na mtu au watu binasfi wakijisifu –majigambo au vivugo.
10. Sifo huasi au kuonyesha thamani ya jamii zinazothamini ujasiri wa kivita, nyingine nasaba tukufu, ufugaji wa mifugo wengi, kilimo au arusi.
11. Sifo hupiga chuku sifa za anayesifiwa

kevowmuchiri answered the question on July 24, 2018 at 12:39


Next: Jadili nyimbo za sifa/sifo
Previous: Orodhesha madhumuni ya kuimba nyimbo za sifa

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions