Orodhesha madhumuni ya kuimba nyimbo za sifa

      

Orodhesha madhumuni ya kuimba nyimbo za sifa.

  

Answers


kelvin
1. Sifo husifu matendo ya viongozi au watu mashujaa katika jamii
2. Hutangaza mafanikio au mchango wa mtu au watu wanaosifiwa kwa jamii, anayeimba sifo hutaja mambo ambayo anayesifiwa alitenda au ametenda.
3. Hukuza uzalendo, sifo huwahimiza vijana kuiga matendo mazuri ya wanaosifiwa, kwa njia hii, watu hujifunza kuionea fahari jamii na kuwa tayari kuitolea mchango wao.
4. Kuweka kumbukumbu au rekodi ya matukio ya kihistoria, wimbo unaomsifu shujaa wa vita, k.m huonyesha vita alivyopigana, alipigana na nani na lini na mbona
5. Huonyesha msimamo na mitazamo ya jamii fulani kuhusu maswala mbalimbali, wimbo unaosifu uzalendo wa mtu fulani, vilevile unaweza kuonyesha chuki kwa usaliti.
6. Hutambua mchango wa watu mbalimbali kwa jamii, sifo hutaja majina ya wanaosifiwa kwa nia ya kutambua na kutambulisha juhudi zao
7. Huburudisha, sifo nyingi hutumbuiza, hutuliza na hupumbaza akili.

kevowmuchiri answered the question on July 24, 2018 at 12:39


Next: Taja sifa zozote mahususi za nyimbo za sifo
Previous: Eleza maana ya hodiya huku ukieleza huimbwa wakati upi

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions