Watu wanaoimba hodiya hunuwia kutimiza lengo lipi?

      

Watu wanaoimba hodiya hunuwia kutimiza lengo lipi?

  

Answers


kelvin
1. Huhimiza watu kutia bidii na kuendeleza kazi bila kufa moyo.
2. Hukashifu uvivu na utegemezi, baadhi ya nyimbo za kazi hukashifu wasiopenda kazi
3. Hurahisisha kazi kwa kupunguza fikra za uchovu, watu wanapofanya kazi wakiimba kazi huonekana kuwa nyepesi na muda kupita kwa kasi.
4. Husawiri imani, mitazamo na thamani za jamii husika kuhusu kazi jamii inathamini kazi gani? Uzembe na bidii kazini huchukuliwaje? Kazi inapewa nafasi gani?
5. Huonyesha changamoto ambayo wafanyakazi hukabiliana nayo katika kazi zao, je, wanahofia nini kazini? Wana matumaini gani katika kazi zao?
6. Hujenga ushirikiano, watu wanapoimba wanapofanya kazi pamoja hujenga ushirikiano; pia huhimizwa katika baadhi ya nyimbo za kazi.

kevowmuchiri answered the question on July 24, 2018 at 12:44


Next: Taja sifa kabambe za hodiya
Previous: Nini madhumuni gani ya kuimba nyimbo za mapenzi?

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions