Nini madhumuni gani ya kuimba nyimbo za mapenzi?

      

Nini madhumuni gani ya kuimba nyimbo za mapenzi?

  

Answers


kelvin
1. Kusifu tabia au umbo la mpenzi, yaani hutaja tabia chanya na umbo zuri la mpenzi.
2. Kutakasa hisia za anayeimba, mwenye mapenzi huweza kutumia nyimbo kutoa hisia zake za huzuni, furaha au kupumbazika kwa kufanya hivi anaweza kupunguza uzito wa hisia alizonazo.
3. Huburudisha, nyimbo za mapenzi huburudisha anayezisikiza.
4. Hukuza ubunifu, nyimbo za mapenzi hubuniwa kwa ubingwa wa hali ya juu ili kuibua hisia za mapenzi, huzuni au huruma.
5. Ni nyenzo ya kupitisha maarifa au elimu, nyimbo za arusi hutumiwa kutoa mawaidha ya unyumba kwa maarusi wapya aidha matarajio ya jamii na majukumu yao mapya kama bibi na bwana hupitishwa kwa nyimbo.

kevowmuchiri answered the question on July 24, 2018 at 12:45


Next: Watu wanaoimba hodiya hunuwia kutimiza lengo lipi?
Previous: Jadili nyimbo za mapenzi huku ukitoa sifa zake

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions