Jadili nyimbo za mapenzi huku ukitoa sifa zake

      

Jadili nyimbo za mapenzi huku ukitoa sifa zake.

  

Answers


kelvin
Nyimbo hizi zinaimbwa kueleza hisia za mapenzi, zinasimamia maoni ya jamii kuhusu mapenzi mtu anaweza kumsifu mpenzi au kusikitika kwa kuachwa na mpenzi, nyimbo hizi huwa na maudhui ya mapenzi.
Sifa
1. Huelezwa kwa maneno matamu yenye hisia nzito.
2. Zinaweza kuwa sifa, yaani zikaimbwa kumsifu mpenzif fulani.
3. Huthibitisha mapenzi.
4. Huwa na maudhui mbalimbali kulingana na lengo la mwimbaji k.m
i) Kuonyesha kusalitiwa au wivu.
ii) Kuomba uchumba.
iii) Kumsifu mpenzi-husifu umbo au hulka yake.
iv) Kutambua uhusiano mzuri na mwenziwe na kumbembeleza mpenzi.

kevowmuchiri answered the question on July 24, 2018 at 12:47


Next: Nini madhumuni gani ya kuimba nyimbo za mapenzi?
Previous: Nyimbo za chekechea zina sifa zipi?

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions