Eleza sifa tano za kimsingi zinazotambulisha sajili ya siasa

      

Eleza sifa tano za kimsingi zinazotambulisha sajili ya siasa.

  

Answers


Peter
Sifa za sajili ya siasa
(a) Matumizi ya msamiati wa kisiasa kama vile uchaguzi, kura, mbunge, sheria n.k
(b) Msamiati wa heshima- Nawaomba wananchi watukufu mnipigie kura
(c) Matumizi ya lugha iliyojaa hadi mfano, mkinichagua nitawajengea hospitali, shule zaidi na kuwapa kazi vijana wote
(d) Wanasiasa wengine huharibu lugha katika uteuzi wao wa msamiati. Mfano hii uchaguzi mpaka mtu aangushwe
(e) Kurudiwarudiwa kwa kauli kama njia ya kusisitiza jambo lisemwalo. Mfano, Mimi nimeleta maendeleo, nikaleta maji, nikaleta stima, nikaleta sipitali…mwataka nani mwingine kweli?
(f) Mazungumzo huendelezwa kwa nafsi ya kwanza. Mfano, Mimi nimewatetea bungeni, nikaungana nanyi hapa, tukashikana mikono mpaka tukapata haki yetu
(g) Matumizi ya maswali ya balagha mfano, Msiponipa kura zenu, nani mwingine?
(h) Kuna matumizi ya mbinu ya tawasifu mfano, Mimi ndiye kiongozi aliyezindua mradi huo, nikamwalika kiongozi wa kitaifa akaja kuufungua kwa sababu anaheshimu kazi yangu nzuri
Musyoxx answered the question on July 25, 2018 at 13:57


Next: THE TEARS OF A SLAVE Adieu, to my native shore, To toss on the boisterous wave; To enjoy my kindred no more, But to weep – the tears...
Previous: Kidagaa kimemwozea (alama 20) 1.…Walimpiga kituku kama nyoka.Nikumbukapo naona fundo chungu moyoni… (a) Eleza muktadha wa dondoo (alama 4) (b) Taja mbinu mbili za lugha...

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions