Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Kidagaa kimemwozea (alama 20) 1.…Walimpiga kituku kama nyoka.Nikumbukapo naona fundo chungu moyoni… (a) Eleza muktadha wa dondoo (alama 4) (b) Taja mbinu mbili za lugha...

      

Kidagaa kimemwozea (alama 20)

1.…Walimpiga kituku kama nyoka.Nikumbukapo naona fundo chungu moyoni…

(a) Eleza muktadha wa dondoo (alama 4)
(b) Taja mbinu mbili za lugha katika dondoo hili (alama 2)
(c) Kwa kurejelea dondoo hili fafanua maudhui yanayojitokeza (alama 2)
(d) Fafanua maudhui uliyotaja hapo juu (c) kwa kutoa mifano kwa riwaya nzima (alama 12)

2.Fafanua mbinu hizi kama zinavyojitokeza katika riwaya. (alama 20)
(a) Barua
(b) Kinaya
(c) Sadfa
(d) Mbinu rejeshi
(e) Majazi

  

Answers


Peter
1.
(a) Msemaji ni Imani
-Msemewa ni Amani
-walikuwa katika kibanda cha Amani
Imani alikuwa akimhadithia Amani sababu ya yeye kusafiri Sokomoko na kutoka nyumbani kwao.
(b) (i) Tashbihi kwa mfano walimpiga kitutu kama nyoka.
(ii) Mbinu rejeshi-Nikumbukapo naona fundo chungu moyoni.
(c ) Ukatili/dhuluma
Kuuliwa kwa mamake Imani na kuchomwa kwa nyumba zao

(i) Yusufu anafungwa jela kwa makosa ambayo hakutenda kwa kusingiziwa kifo cha chichiri Hamadi
(ii) Amani anadhulumiwa kwa sababu ya unyonge.Familia yake inanyanganwa shamba
(iii) Amani na Imani kudhulumiwa na askari wa Mtemi Nasaba Bora wakiwa seli
(iv) Mtemi Nasaba Bora kutumia askari kumpiga na kumuua mamake Imani
(v) Amani anaonewa gere na wanafunzi wenzake wanaficha karatasi za uchochezi kwa chumba chake na kugungwa kipindi cha miaka mitatu
(vi) Bob Dj kudhulumiwa na Mtemi Bora kwa kutopelekwahospitali baada ya kung’atwa na mbwa.
(vii) Matuko weye kudhulumiwa na askari wa Mtemi kwa kushikwa kwa nguvu na kupelekwa seli baada ya kusema ukweli kuhusu Nasaba Bora.
(viii) Chwechwe anadhulumiwa na serikali ya Tomoko baada ya kuvunjika fupaja
(ix) Majisifu kumwachia Dora malezi ya watoto wao walemavu
2.
(i) Barua
-Barua ya majisifu kutoka chuo kikuu cha mkokotoni kumwalika kutoa mhadhara kwa wanafunzi kuhusu kitabu chake cha kidagaa kimemwozea
-Barua ya Ben Bella kwa Mashaka kuvunja uhisiano
-Barua ya madhubuti kwa Mtemi Nasaba Bora kumjulisha kwamba alikamilisha masomo yake na alikuwa tayari kusafiri.Pia alimwambia kwamba asimamishe mipango za kumtafutia kazi.
-Barua ya Lowela kwa Mtemi Nasaba Bora akimtishia kutoboa siri asipowaachilia Amani na Imani
(ii) Kinaya
_ Ni kinaya kwamba uso wa Imani unaonyesha tabasamu ilhali moyoni ana huzuni
-Ni kinaya kwamba Mitchelle anamwagiza Majununi kujenga jumba kubwa baadaye anaikataa
-Kinaya kwamba zahanati ya Nasaba Bora inajulikana kama mahali watu wameenda kufia badala ya kupata nafuu..kwa mfano kitoto uhuru
-Nasaba Bora anamwamba Amani kuwa ni mwizi ilhali yeye ndiye
(iii) Sadfa
-Imani na Amani wanakutana kisadfa ziwa Mawewa wote wakiwa safarini kuelekea sokomoko kusaka ajira.
-Imani na Amani wanakutana na Bob Dj pale mto kiberenge na anawapeleka kwa ndugu wawili Nasaba Bora na majisifu
-Amani na Imani wanafika sokomoko kwa Nasaba Bora anapohitaji mchungaji na majisifu kijakazi
_Amani kupatikana na Nasaba Bora chumbani wakiwa na mkewe Bi.Zuhura.
Mbinu rejeshi
(a) Kisa cha Mitchelle na Majununi tunaona usaliti wa Mitchelle
(b) Kisa cha Imani kusimulia Amani kifo cha mamake na kuchomwa kwa nyumba yao
(c) Kisa cha mtemi kununua gari jipya na kumuua paka aliyekula nyama
(d) Tunarudishwa nyuma kurejelea mwiko wa kunywa maji yam to Kiberenge.
(e) Mtemi Nasaba Bora anakumbuka maisha yao wakiwa wadogo babake akiwa kasisi
Majazi
Madhubuti- maana kitu chenye Imara.Anakataa kutafutiwa kazi kwa njia ya hongo.
Majisifu-Ni majigambo.Anajiona kuwa mwandishi maruufu na bora kisarufi
Mashaka-Taabu.Anaachwa na Ben Bella na hata kuwa wazimu
Amani-Mtulivu.anamsamehe Mtemi Bora baada ya kujua ukweli na kutolipiza kisasi.

Musyoxx answered the question on July 25, 2018 at 14:03


Next: Eleza sifa tano za kimsingi zinazotambulisha sajili ya siasa
Previous: TAMTHILIA YA MSTAHIKI MEYA “Najua ni kazi ila usisahau pia kwamba wafanyikazi wamegoma.” (i) Fafanua muktadha wa dondoo hili. (alama 4) ...

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions