TAMTHILIA YA MSTAHIKI MEYA “Najua ni kazi ila usisahau pia kwamba wafanyikazi wamegoma.” (i) Fafanua muktadha wa dondoo hili. (alama 4) ...

      

TAMTHILIA YA MSTAHIKI MEYA
“Najua ni kazi ila usisahau pia kwamba wafanyikazi wamegoma.”
(i) Fafanua muktadha wa dondoo hili. (alama 4)

(ii) Wahusika wawili wanaohusishwa na dondoo hili wamebaidika kama ardhi na `
mbingu. Thibitisha. (alama 16)

  

Answers


Peter
4. (a)
• Msemaji ni Diwani III/Bw. Kheri/Bw. Uchumi
• Anamwambia Meya Sosi
• Walikuwa ofisini kwa Meya
• Meya alikuwa amemwita kutaka atekeleze nyongeza ya mishahara ya wafanyakazi
• Meya anadai kuwa uwakilishi/udiwani ulikuwa kazi
(b) Wahusika hawa ni Meya na Diwani III
• Meya ni katili-anatumia askari kuwapiga na kuwatawanya wafanyakazi wanaodai haki. Diwani III ni mwenye utu- anajali maslahi ya wafanyakazi na kutaka wasikilizwe
• Meya ni mbaguzi/mwenye mapendeleo- anawaongeza madiwani mshahara na kuwapuuza wafanyikazi. Diwani III ni mpenda usawa- anapendekeza madiwani na wafanyakazi wapate nyongeza wote.
• Meya ni mwongo/mdanganyifu- anadai dawa zimeagizwa na zi njiani zaja. Diwani III ni mkweli. Anaeleza wazi kuwa ahadi za Meya za kuagiza dawa zilikuwa ni uongo.
• Meya ni mwoga. Anaogopa kutiwa kizuizini. Anaposhikwa na askari anazimia. Diwani III ni jasiri/mkakamavu- anapinga waiwazi maamuzi ya kueneza propaganda kuwa Baraza la Cheneo limejitolea kuwaletea demokrasia
• Meya ni mwenye kiburi/majivuno- anadai kuwa wanacheneo wanaridhika naye na wangeendelea kumchagua. Diwani III ni mwenye heshima/mnyenyekevu- kila anapokutana na Meya, anamwita MstahikiMeya. Anapopinga hoja anafanya hivyo kwa heshima na kutoa sababu za kuridhisha.
• Meya ni msaliti- anawasaliti wanacheneo kwa kutowapatia mahitaji yao ya kimsingi kama vile chakula, elimu bora, matibabu na kazi. Diwanii III ni mzalendo- anapinga maamuzi yanayochangia kufilisi hazinz ya baraza/ufujaji wa mali ya umma.
• Meye ni mjinga- hatambui unafiki wa Bili na Diwani I na II. Hawa wanamdanganya ili wafaidi. Diwani III ni mwerevu- anatambua kuwa watu wameerevuka na lazima uongozi uweze kutahadhari. Anatambua Meya anapofushwa na viongozi wanafiki.
• Meya ni fisadi- anatumia cheo chake ili kunyakua viwanja vinane na kumgawia rafikiye Bili vinne. Diwani III ni mwadilifu- anakataa kushiriki njama za Meya na madiwani wenzake kufilisi Baraza.
• Meya ni mbadhirifu- anatumia fedha za umma ovyo. Anashiriki starehe katika hoteli, kuidhinisha malipo haramu na kuandaa sherehe ghali. Diwani III ni mwangalifu/mwekevu- anapinga matumizi mabaya ya pesa za umma kwa mfano nyongeza ya mishahara kwa madiwani na kutotozwa kodi kwao

Musyoxx answered the question on July 25, 2018 at 14:05


Next: Kidagaa kimemwozea (alama 20) 1.…Walimpiga kituku kama nyoka.Nikumbukapo naona fundo chungu moyoni… (a) Eleza muktadha wa dondoo (alama 4) (b) Taja mbinu mbili za lugha...
Previous: TAMTHILIA YA MSTAHIKI MEYA “Unaona sasa?Mlinidanganya.”Kauli hii ni idhibati tosha kuwa,Mstahiki Meya alidanganyika na kuongozwa na falsafa zisizo na mashiko katika uongozi wake.Tetea ukweli huu. (alama 20)

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions