Taja sifa zozote nne za majigambo

      

Taja sifa zozote nne za majigambo.

  

Answers


KELVIN
i. Hutungwa na kughanwa na mhusika mwenyewe.
ii. Hutungwa kwa usanii mkubwa, anayejigamba hutumia sitiari, ishara, takriri na tashbihi.
iii. Anayejigamba hujitumia kivugo kufuatia tukio mahususi katika maisha yake, anaweza kuongea kuhusu siku za jandoni, ndoa au kuoa, kutoka vitani, michezo, kesi au jambo kali.
iv. Kwa kawaida hutungwa na kughanwa na wanawake.
v. Huwa na matumizi ya chuku kwa kiasi kikubwa, anayejigamba hujisifu kupita kiasi kwa kutaja mafanikio au mchango wake. Anaweza kuahidi kuleta mafanikio makubwa kuliko yale tayari ameletea jamii.
vi. Hutolewa kwa nafsi ya kwanza maadam anayejigamba ni mshairi mwenyewe.
vii. Anyejigamba huweza kubeba baadhi ya vifaa vyake vya kazi au vinavyoonyesha jambo analojisifia. Aidha anaweza kuvaa maleba yanayooana na kazi au jambo ambalo anajisifia
viii. Kwa kawaida, hutungwa papo hapo hata hiyo mengine huandikwa ili kughanwa baadaye katika hafla fulani k.v arusi.
ix. Anayejisifu hutaja usuli wake wa kinasaba, katika baadhi ya jamii anayejigamba huhitajika kutaja na kusifu nasaba au ukoo wake, upande wa baba na mama kwa majina yake halisi.
x. Wanaojigamba nao huwa walumbi au washauri wanaofahamu wanalolitunga.
xi. Maudhui makuu ni ushujaa

kalvinspartan answered the question on July 30, 2018 at 16:05


Next: Highlight the techniques of assessing children in ECDE
Previous: Majigambo yana umuhimu gani katika jamii

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions