Majigambo yana umuhimu gani katika jamii

      

Majigambo yana umuhimu gani katika jamii.

  

Answers


KELVIN
a) Hukuza ubunifu –kadri mtu anavyotunga na kughani majigambo ndivyo anavyoimarisha uwezo wa kubuni mitindo mipya ya utunzi na uwasilishaji.
b) Hukuza ufasaha wa lugha watunzi wengine wa majigambo huwa walumbi.
c) Ni nyenzo ya burudani, huangua waliohudhuria sherehe ambapo yanatolewa.
d) Hudumisha utu na utambulisha mwanamume katika familia, kwa sababu ya uchokozi uliokuwa katika jamii, ilikwa muhimu kwa wanaume katika familia kuwa jasiri, wakakamavu na mashujaa ili kutetea jamii zao. Kupitia kwa majigambo wanaume walidhihirisha nafasi zao katika jamii.
e) Nyenzo ya kufanya watu waheshimiwe, hudumisha ari ya kuwafanya wanaume kutaka kuwa mashujaa mtu alipofanya kitendo cha ushujaa, alijigamba na kuheshimiwa na kila mtu alitaka kufanya jambo la kishujaa ili ajigambe na kuheshimiwa

kalvinspartan answered the question on July 30, 2018 at 16:07


Next: Taja sifa zozote nne za majigambo
Previous: Eleza maana ya tondozi

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions