Semi huwa na malengo yepi katika jamii

      

Semi huwa na malengo yepi katika jamii.

  

Answers


KELVIN
a) Semi huelimisha, vitendawili, methali, mafumbo na nahau zote hutoa mafunzo ya aina Fulani; methali “mwenda pole hajikwai “hutoa maarifa ya kufanya mambo bila pupa.
b) Hukuza uwezo wa kufikiria, vitendawili, methali na mafumbo humhitaji mtu kufikiria ili kupata ujumbe uliofumbwa.
c) Hutambulisha jamii na wanajamii, kila jamii huwa na semi mahususi zinazohusu shughuli zake, misimu kwa mfano hutumiwa na kundi fulani katika jamii.Methali mkulima ni mmoja walaji ni wengi inatambulisha jamii inayohusika katika kilimo, kitendawili kimoja kinaweza kuwa na majibu tofauti kutegemea jamii na mazingira yake.
d) Hukuza utangamano, wakati wa kutegeana vitendawili; kwa mfano watu huja pamoja aidha misimu hujenga uhusiano wa karibu miongoni mwa watu wanaoitumia, lakabu nazo hutumiwa na watu walio na uhusiano wa karibu.
e) Huburudisha, baada ya shughuli za kazi watu hujumuika pamoja katika vikao vya kujiburudisha ambapo hutegeana vitendawili na hushiriki katika vitanza ndimi ili kutuliza bongo na kusisimka.
f) Huhifadhi utamaduni, semi hufumbata desturi za jamii zinapopitishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine, utamaduni huo hufunzwa na kuhifadhiwa.
g) Husawiri mitazamo ya jamii kuhusu masuala Fulani, je, jamii inachukia nini? Inahimiza nini? Kupitia kwa methali bidii ya mja haiondoi kudura tunafahamishwa kwamba jamii hii inaamini kuwa binadamu yumo chini ya uwezo wa Mungu nahau, lakabu, vitendawili na mafumbo pia hufumbata tajiriba ya jamii.
h) Hututasfidia lugha, nahau, misemo, misimu na lakabu hutumiwa badala ya msamiati mkali /wenye aibu, badala ya kusema ‘kuzaa’tunasema ‘kujifungua’
i) Hukuza lugha, semi huyapa maneno maana mpya au maana ya ziada. Misimu huweza kukubaliwa na kuwa nahau rasmi za lugha kwa njia hii msamiati wa lugha hupanuliwa.

kalvinspartan answered the question on July 30, 2018 at 16:13


Next: Fafanua maana ya pembeziji
Previous: Eleza maana ya methali

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions