Eleza maana ya methali

      

Eleza maana ya methali

  

Answers


KELVIN
Methali ni semi fupifupi za kimapokeo zenye kueleza fikira, maarifa, hekima na mafunzo yanayotokana na uzoefu wa jamii mahususi. Methali hutumia taswira na mafumbo, chukulia kwa mfano, fimbo ya mbali haiui nyoka, utungo huu ni mfupi na unatumia neno ‘fimbo kama fumbo la ‘suluhisho’
Methali ni tanzu tegemezi kama ilivyotajwa kutumika kwake hutegemea tanzu nyingine. Methali hutokea katika mazungumzo mazito kama vile kutoa mawaidha au kama kielelezo na kifupisho cha hadithi si utanzu unaoweza kujisimamia kama tanzu nyingine kama vile hadhithi, ushairi au mazungumzo.

kalvinspartan answered the question on July 30, 2018 at 16:13


Next: Semi huwa na malengo yepi katika jamii
Previous: Eleza sifa tano za methali

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions