Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Eleza sifa tano za methali

      

Eleza sifa tano za methali.

  

Answers


KELVIN
? Methali ni kauli fupi ambazo hutolewa kwa mtindo wa kishairi kinyume na jinsi kauli za kawaida zinavyowasilishwa.
? Methali zina sifa za kishairi, huwa na vipande vyenye mizani inayolingana na kwamba ni mshororo mmoja.
? Maudhui katika methali huchotwa katika jamii zinamozaliwa, maudhui hutokana na tajriba na mambo yanayoathiri jamii.
? Huwa na muundo maalumu wenye sehemu mbili, kwa mfano. Aliye juu, mngoje chini sehemu ya kwanza hudokeza wazo na ya pili hulikamilisha kwa kukubali au kukataa.
? Hujengwa kwa tamathali nyingine za usemi na mbinu za lugha kama vile kinaya, taswira na takriri, methali kukopa arusi kulipa matanga imejengwa kwa sitiari.
? Methali hueleweka na jamii iliyozibuni kwani hubuniwa kutokana na mazingira ya jamii husika.
? Methali zina sifa ya utegemezi na huingiliana na tanzu nyingine za fasihi.
? Hutumiwa mwishoni mwa ngano kufupisha maadili ya ngano hiyo.
? Hutumiwa kubuni lakabu, mtu ambaye huwasaliti marafiki anaweza kuitwa ‘kikulacho’ kutokana na methali ‘kikulacho ki nguoni mwako’
? Hutumiwa katika tanzu za kimaandishi kama vile riwaya na tamthilia ili kuongeza ladha katika usimulizi.
? Hutumiwa katika mazungumzo ya kawaida na ulumbi kuleta mvuto.
? Hutumiwa katika nyimbo na mashairi
? Hutumika katika hotuba rasmi au hata mahakamani mshtakiwa, mlalamishi na mahakimu wanaweza kutoa maoni yao kutumia methali.
? Hutumika katika kutoa mawaidha
? Methali huelezea ukweli ambao unakubalika na jamii ambao imebuniwa
? Tofauti na vitendawili ,methali hazina muktadha maalumu wa kutolewa .hazitengewi vikao vya kutolewa
? methali ni mali ya jamii, kama tanzu nyingine za faihi simulizi hakuna anayeweza kudai kumiliki methali
? methali huambatana na mazingira ya jamii iliyozizaa, hulka, itikadi, tamaduni na tajriba zake busara fulani huwasilishwa kutegemea mazingira ya jamii kwa mfano.
Ulingo wa kwake haulindi manda
Kamba ya mbali haifungi kuni
Fimbo ya mbali haiui nyoka
? methali zina matumizi mapana.methali moja huweza kuwa na majukumu mbalimbali kama vile kuonya, kuelekeza na kufunza.
? Methali huwa na maana ya ndani na nje, maana ya nje hutokana na maana halisi ya maneno yaliyoiunda. Vilevile, methali hupewa maana ya ndani yenye fumbo lililofumbwa na maneno yanaoiunda.

kalvinspartan answered the question on July 30, 2018 at 16:15


Next: Eleza maana ya methali
Previous: Methali hunuwia madhumuni yapi katika jamii

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions