Methali hunuwia madhumuni yapi katika jamii

      

Methali hunuwia madhumuni yapi katika jamii.

  

Answers


KELVIN
a) Huelimisha, methali hutumiwa kupitisha maarifa ya kijamii kwa wanajami. Abebwaye hujikaza huonyesha kuwa unapopata usaidizi nawe pia jikaze kutia bidii, usingoje tu usaidizi.
b) Huadilisha. methali hufunza maadili kama uvumilivu kwa mfano ‘mstahimilivu hula mbivu’
c) Husawiri mitazamo na falsafa za jamii. Fulani kuhusu masuala mbaliimbali. Je, jamii inapenda nini? Inachukia nini? Methali ucha mungu si kilemba cheupe hudhihirisha kuwa jamii huchukia unafiki.
d) Hutambulisha jamii, kila jamii ina methali zake maalum zinazoitambulisha.
e) Huongeza ladha katika mazungumzo na maandili, mazungumzo na maandishi yenye matumizi mazuri ya methali huvutia.
f) Hubudisha, katika jamii nyingine, methali hutengewa vipindi vya kutolewa na makundi yanayoshindana, hii ni njia mojawapo ya kutuliza bongo.
g) Hurithisha utamaduni wa jamii, methali ni zao la utamaduni husika na hupitishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine hivyo utamaduni huweza kurithiwa.
h) Hufariji, methali huwatuliza na kuwaliwaza watu wanapokabiliana na matukio au hali zinazohuzunisha, kwa mfano hakuna refu lisilo na ncha.
i) Hukuza uwezo wa kufikiri, mtu huhitajika afikiri kwa makini na kuoanisha msamiati uliotumika kwa hali ya maisha ili kupata maana.
j) Hukuza ushirikiano na mshikamano wa jamii. Katika jamii ambazo methali hutengewa vikao, watu hujumuika pamoja hivyo kukuza ushirikiano na mshikamano.

kalvinspartan answered the question on July 30, 2018 at 16:16


Next: Eleza sifa tano za methali
Previous: Methali yaweza kuanishwa vipande tofauti. Eleza

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions