Methali yaweza kuanishwa vipande tofauti. Eleza

      

Methali yaweza kuanishwa vipande tofauti. Eleza

  

Answers


KELVIN
1. Muktadha
Ile kuelewa methali, ni muhimu kujua mazingira, tamaduni na hali zilizozizaa methali hizo methali ambazo zimezaliwa katika muktadha au mazingira sawa huweza kuwekwa katika kundi moja.
2. Maudhui
Maudhui na fani ndiyo hutawala methali, maudhui katika methali ni mengi na mapana kama zilivyo jamii na shughuli zao, methali ambazo huwa na maudhui sawa huwekwa katika kundi moja, baadhi ya maudhui yanayojitokeza katika methali za Kiswahili ni ya
a) Malezi
i. Mchelea mwana kulia hulia mwenyewe
ii. Samaki mkunje angali mbichi
iii. Asiyefunzwa na mamake hufunzwa na ulimwengu.
b) Kazi
i) Kazi mbi si mchezo mwema.
ii) Mchagua jembe si mkulima.
iii) Kazi ya bakuli husiri.
v) Kazi isiyo faidi kutenda si ada.
III. Ushirikiano
i) Kidole kimoja hakivunji chawa.
ii) Jifya moja haliinjiki chungu.
(iii) Umoja ni nguvu utengano udhaifu.
3. Mtindo au fani
Mbali na maudhui, methali hutawaliwa na fani pia. Fani katika methali hudhihirika katika muundo, tamathali za semi na taswira inayoibuliwa, methali ambazo huundwa kwa kutumia fani sawa huweza kuwekwa katika kundi moja. Methali zifuatazo zimeundwa kwa kutumia kweli kinzani
a) Simba mwenda pole ndiye mla nyama.
b) Kuinamako ndiko kuinukako.
4. Jukumu
Methali huweza kuanishwa kulingana na majukumu yake. Je, methali inasifu, inakashifu, inahimiza, inaonya ama inafariji? Methali zifuatazo hutumiwa kuonya:
a) Mwenye pupa hadiriki kula tamu.
b) Asiyeangalia huishia ningalijua.
c) Usione kwenda mbele kurudi nyuma si kazi.
5. Maana
a) Methali zote zenye maana sawa huweza kuwekwa katika kundi moja, kwa mfano.
I. Damu ni nzito kuliko maji
i. Meno ya mbwa hayaumani
ii. Mtoto wa nyoka ni nyoka
iii. Mwana wa mhunzi asiposana, huvukuta.
b) Methali zenye maana zinazokinzana pia zinaweza kuainishwa pamoja, kwa mfano. Mvumilivu hula mbivu. Ngoja ngoja huumiza matumbo. Mtu pweke ni uvundo. Nahodha wengi chombo huenda mrama.

kalvinspartan answered the question on July 30, 2018 at 16:18


Next: Methali hunuwia madhumuni yapi katika jamii
Previous: Huku ukitolea mifano eleza maana ya sitiari

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions