Taja sifa zozote tano za vitendawili

      

Taja sifa zozote tano za vitendawili.

  

Answers


KELVIN
a) Kwa kawaida, vitendawili ni semi fupifupi zinazotumia lugha ya mkato.kwa mfano ’pa’funika ‘pa’funika (jibu; nyayo wakati wa kutembea )
b) Vitendawili hutolewa kwa hadhira ili vifumbuliwe hivyo, hadhira yake ni hai na tendi.
c) Hutumia lugha ya picha au taswira na vina ukwasi wa tamathali za semi.
d) Vitendawili huhitaji watu au makundi mawili ili kukamilisha uwasilishaji wavyo mtu wa kwanza hutega na mwenzake hutegua.
e) Vitendawili huwa na muundo au fumyula maalumu ya uwasilishaji kwa mfano
Mtegaji: kitendawili
Mteguaji: tega!
Mtegaji: nyumba yangu haina mlango
Mteguaji: yai
f) Vitendawili huwasilisha kwa mtindo wa majibizano kati ya mtegaji na mteguaji mteguaji akishindwa kutegua, huhitajika kutoa mji ndipo kupewa jibu na mtegaji
g) Kitendawili ni fumbo au swali liilofichika ambalo huhitaji jibu.
h) Fumbo au jibu la kitendawili hufahamika tu na jamii ambamo kitendawili hicho kimezaliwa, kitendawili kinaweza kuwa na majibu mawili kutegemea mazingira ya jamii kwa mfano, vitendawili vifuatavyo huweza kuwa na jibu zaidi ya moja.
i) Wanangu wawili husabihiana majibu tui na maziwa; unga na majivu.
iii) Mwarabu kasimama kwa mguu mmoja majibu uyoga; mwavuli.
j) Vitendaili ni sanaa ambayo kwa kiasi kikubwa hutegemea uwezo wa mtu kutambua na kuhusisha au kulinganisha vitu katika mazingira yake, kwa mfano ili kufumbua fumbo la kitendawili mbili mbili hadi pwani, lazima mtu aweze kuhusiaha vitu viwili ambavyo daima hufanya jambo pamoja (jibu macho ) macho hutazama pamoja, hulala pamoja na hulia pamoja.
k) Vitendawili huingiliana na tanzu na vipera vingine vya fasihi simuliza kwa mfano ngano za mtanziko hutumia vitendawili, hasa katika fomyula ya ufunguzi wa ngano. Aidha vitendawili hutangulia vikao vya kusimulia hadithi au hutegwa baada ya vikao hivyo.
l) Vitendawili hubadilika kutegemea wakati au kipindi cha kihistoria na maendeleo ya jamii, kitendawili kimoja kinaweza kuundwa au kutolewa kwa maneno tofauti kulingana na kipindi cha wakati kinapotumiwa kwa mfano.
Mwarabu wangu nimemtupa biwini (machicha ya nazi)
Mzungu katupwa jalalani (machicha ya nazi) maneno tofauti (mwarabu na mzungu) katika vitendawili hivi viwili ambavyo vina jibu moja yanaonyesha viliathiriwa na nyakati tofauti za kihistoria.
m) Vitendawili ni sanaa inayotendwa kwa hivyo hujisimamia yenyewe tofauti na methali ambazo kwa kawaida ni sanaa tegemezi. Hutegewa vikao maalumu na kutolewa.
n) Kimaudhui, vitendawili hushughulikia masuala katika nyanja zote za maisha ya binadamu na mzingira yake. Maudhui haya hutofautiana katika jamii mbalimbali ingawa baadhi yao huingiliwa

kalvinspartan answered the question on July 30, 2018 at 17:35


Next: Eleza maana ya vitendawili
Previous: Je vitendawili huwa na umuhimu gani katika jamii

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions