Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Je vitendawili huwa na umuhimu gani katika jamii

      

Je vitendawili huwa na umuhimu gani katika jamii.

  

Answers


KELVIN
a) Vitendawili huelimisha, vitendawili hujumuisha masuala mengi katika mazingira ya jamii.
b) Hali hii inavifanya kuwa na uwezo mkubwa wa kuelimisha watu kuhusu mazingira yao aidha mtu akikosa jibu haadhibiwi zaidi ya kutoa mji.
c) Huburudisha.vitendawili huwapumbaza na kuwapumzisha wanaoshiriki katika utegaji ua utegauaji wavyo.
d) Hufundisha kaida na maadili ya jamii, vitendawili huwa na utaratibu fulani unaofuatwa na ambao washiriki wanapaswa kuuheshimu na kuuzingatia, hii ni njia moja ya kuadilisha kwa kuwa kila jambo maishani lina kaida zake zinazoheshimiwa.
e) Hukuza ubunifu na stadi ya kufikiri haraka, mteguaji wa kitendawili sharti afikiri na kuoanisha yaliyotajwa na mazingira yake ili kupata jawabu.Vitendawili hukuza ari ya kufikiria na kudadisi mazingira.
f) Vitendawili hudhihaki na kukejeli watu, hali au tabia hasi katika jamii.hukashifu matendo hasi na kusifu yale chanya
g) Husawiri mitazamo na itikadi ya jamii kuhusu hulka fulani, kwa mfano nyumbani kwetu kuna papai lililoiva sana lakini nashindwa kulichuma (jibu: kaka au dada) inaonyesha kuwa ndoa kati ya dada na kaka hairuhusiwi.
h) Hukuza uwezo wa kukumbuka vitendawili hutumiwa kama chemshabongo ya kujaribu uwezo wa mtu kukumbuka na kuhusisha mambo
i) Huleta umoja na ushirikiano katika jamii, watu hujumuika wakati wa kutegeana vitendawili kwa njia hiyo utangamano huimarika.
j) Hutambulisha jamii kila jamii huwa na vitendawili vinavyoonyesha mazoea, hali, tajriba na mazingira ya jamii husika.
k) Huchochea tabia ya udadisi, uzoefu wa kutafuta kiini cha kitendawili hujenga tabia ya kutaka kufichua jambo lililofichika kwa kujaribu kupata jibu la jambo ktika kitendawili wanajamii huimarisha ari yao kutafiti mambo ili kubaini kiini chake.
l) Vitendawili hukuza na kusambaza ujuzi wa lugha, vitendawili vina ukwasi mkubwa wa lugha na tamathali za semi kwa hivyo ni nyenzo kuu ya kukuza na kusambaza maswala ya lugha katika jamii.

kalvinspartan answered the question on July 30, 2018 at 17:36


Next: Taja sifa zozote tano za vitendawili
Previous: Eleza mtindo wa vitendawili

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions