Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Taja sifa nne kuu za misimu

      

Taja sifa nne kuu za misimu

  

Answers


KELVIN
a) Misimu ni semi au msamiati ambao huzuka na kutoweka baada ya muda Fulani.
b) Hutumiwa na wanajamii katika mawasiliano ya makundi fulani k.m kuna misimu ya vijana ya wafanyakazi katika vyombo vya usafiri na hata ya watoto.
c) Hutumiwa na wanajamii katika mawasiliano yao katika kipindi fulani cha wakati na mahali fulani
d) Ingawa misimu huzuka na kutoweka baada ya muda, baadhi ya misimu hudumu na kukubalika kama semi au msamiati sanifu wa lugha husika kwa mfano neno chai (kwa maana ya hongo ) lilianza kama msimu, kisha likashika na kukubalika kama msemo sanifu.
e) Msimu hupata maana yake kutoka kwa watumiaji pamoja na muktadha wa mahali na wakati, kwa mfano neno sare ni msimu uliopata maana katika sekta ya usafiri wa matatu likimaanisha kubebwa bila malipo.

kalvinspartan answered the question on July 30, 2018 at 17:50


Next: Misimu ina dhima gani?
Previous: Eleza njia tofauti za kuanisha misimu

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions