Lakabu zina umuhimu gani katika jamii

      

Lakabu zina umuhimu gani katika jamii.

  

Answers


KELVIN
a) Kusifiwa kwa matendo chanya ya mhusika.
b) Hukashifu au kukejeli matendo mabaya ya mhusika.
c) Ni kitambulisho cha mhusika husawiri tabia au hali ya mtu fulani ka maneno machache.
d) Hutumiwa kama ishara ya hesima katika jamii ambamo kumtaja mkazamwana kwa jina lake ni mwiko, baba mkwe huibua lakabu ya kumrejelea mkazamwanawe.
e) Hutumiwa na baadhi ya wahusika kuficha utambulisho wao baadhi ya waandishi hujibandika majina ya uandishi ili kuficha majina yao halisi.
f) Hutumiwa na wahusika kujigamba na kujinaki katika majigambo, anayejigamba hujipa lakabu ili kujinaki na kuonyesh ubingwa wake.
g) Hutumiwa kuhifadhi siri wakati mwingine watu humpa mtu fulani lakabu ili wanapomrejelea isijulikane ni nani.
h) Hukuza uhusiano bora hasa miongoni mwa watani katika kutaniana watu huweza kubandikana majina.
i) Hutumiwa kuondoa urasmi katika mahusiano ya kijamii.

kalvinspartan answered the question on August 5, 2018 at 12:28


Next: Taja sifa tano mahususi za lakabu
Previous: Eleza maana ya vitanza ndimi

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions