Eleza maana ya nahau

      

Eleza maana ya nahau.

  

Answers


KELVIN
Nahau ni fungu la maneno ya kawaida lenye maana ambayo haitokani moja kwa moja na maana za maneno yaliyoziunda, nahau piga kalamu si kuchapa kalamu bali ni ‘kufuta mtu kazi’
Mifano mingine ni.
Piga maji- Lewa.
Kujitia hamnazo – Kujifanya hujui.
Kukata kamba- Kufa.
Kunja jamvi- Maliza shughuli.
Kwenda nguu- Kukata tama.
Piga vijembe- Kusema kwa mafumbo.
Kumwaga unga- Kuachishwa kazi.
Ndege mbaya- Bahati mbaya.
Kupata jiko- Kuoa.
Shingo upande- Bila kutaka.

kalvinspartan answered the question on August 5, 2018 at 12:37


Next: Eleza dhima ya mafumbo
Previous: Eleza dhima ya nahua katika fasihi

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions