Eleza maana ya misemo huku ukitolea mifano

      

Eleza maana ya misemo huku ukitolea mifano.

  

Answers


KELVIN
Misemo ni semi ambazo zinabeba ukweli wa kijumla, hutumika kueleza mambo mbalimbali yanayokubali ukweli huo. Misemo hutumiwa kutoa ujumbe kwa muhtasari mfano zaidi.
i. Binadamu ni udongo –kumaanisha binadamu aliumbwa kwa udongo na hufa na kurudi udongoni.
ii. Mwili haujengwi kwa mbao-mtu lazima ale ili apate kujenga mwili au kunenepa hauwezi kujengwa kwa mbao.
iii. Umaskini si kilema-kumaanisha kuwa mambo hubadilika ukizaliwa katika umaskini si lazima uishi na ufe ukiwa maskini.
iv. Lila na fila havitangamani –ubaya na wema hayaendi pamoja.
v. Ndio kwanza mkoka ualike maua –kumaanisha ndio mambo yamezidi kushika kasi.
vi. Mgomba haupandwi changaraweni ukamea –jambo njema halifanywi mahali pabaya likapendeza.
Baadhi ya misemo hutumiwa kama methali kwa mfano, umoja ni nguvu utengano ni udhaifu.

kalvinspartan answered the question on August 5, 2018 at 12:39


Next: Eleza dhima ya nahua katika fasihi
Previous: Mkusanyaji wa fasihi anafaa kufuata hatua zipi

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions