Mkusanyaji wa fasihi anafaa kufuata hatua zipi

      

Mkusanyaji wa fasihi anafaa kufuata hatua zipi.

  

Answers


KELVIN
a) Kujiadaa – hapa mtu anatakiwa kuzingatia
? Mada ya utafiti –anatafiti kuhusu nini?
? Mawanda ya utafiti – Kama ni kitendawili anatafiti fani? Aina?
? Walengwa – jamii ipi? Wenye umri gani?
? Kipindi cha utafiti – utaanza na kutarajia kumaliza lini?
? Kuomba kibali cha utafiti kutoka kwa taasisi husika k.v wizara ya elimu
? Mbinu za ukusanyaji na kuhifadhi data, je atatumia: Hojaji au mahojiano je, vifaa hivi vi tayari?
? Gharama ya utafiti –je, atatumia kiasi gani cha pesa? Nani atafadhili utafiti?
b) Utafiti na ukusanyaji wa data –mtafiti anaweza kukusanya data kupitia hojaji, mahojiano, kushiriki au kutazama.
c) Rekodi ya data –kuna njia mbalimbali za kurekodi data basi vifaa hivi sharti viwen tayari kabla ya utafiti.
d) Kuchunguza upana wa data/maelezo yaliyotolewa na walengwa na kuyanakili ili kuyachunganua baadaye.
e) Uchanganuzi na kufasiri wa data –huchanganuliwa kulingana na vigezo vya uchanganuzi alivyoweka na kulingana na mada yake. Matokeo hutumiwa kutoa hitimisho na mapendekezo kuhusu mada ya utafiti.

kalvinspartan answered the question on August 5, 2018 at 12:41


Next: Eleza maana ya misemo huku ukitolea mifano
Previous: Eleza maana ya kushiriki kama njia mojawapo ya kukusanya fasihi huku ukitoa umuhimu wake

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions