Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Eleza maana ya kushiriki kama njia mojawapo ya kukusanya fasihi huku ukitoa umuhimu wake

      

Eleza maana ya kushiriki kama njia mojawapo ya kukusanya fasihi huku ukitoa umuhimu wake.

  

Answers


KELVIN
Mkusanyaji aweza kujiunga na jamii kwa kushiriki katika ngoma, soga na masimulizi ya hadithi na tanzu nyingine hapa anayekusanya data ya fasihi simulizi haulizi bali hujirekodia anachokibaini katika ushirika huo.
Umuhimu wa kushiriki
a) Mtafiti huja karibu zaidi na jamii na hupata habari za kuaminika moja kwa moja
b) Ni njia bora ya kukusanya habari kwa watu wasiojua kusoma na kuandika ama wanaona vigumu kujieleza moja kwa moja.
c) Ni rahisi kwa mtafiti kuuliza maswali kuhusu kipera kinachowasilishwa mathalani anaweza kuuliza kuhusu kipidi ambamo wimbo fulani uliimbwa au hadhira mahususi ambayo ilitambiwa aina fulani ya ngano.
d) Mtafiti huweza kunakili anayosikia au kuona, hivyo kuhifadhi sifa za kiimbo, toni na ishara.
e) Mtafiti hupata taathira na hisia halisi ya yanayowasilishwa kwani anakabiliana wazi na watendaji halisi huelewa zaidi.
f) Mtafiti huweza kuthibitisha aliyokusanya kwa hojaji au mahojiano kwa kuyahakiki
g) Kusiriki hukuza utangamano kati ya mtafiti na wanajamii.ni rahisi kwa mtafiti kupata majibu ya masuala anayotafiti kwa kushiriki na kutangamana na wanajamii.

kalvinspartan answered the question on August 5, 2018 at 12:42


Next: Mkusanyaji wa fasihi anafaa kufuata hatua zipi
Previous: Eleza udhaifu wa kushiriki kama njia ya kukusanya fasihi

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions