Eleza udhaifu wa kushiriki kama njia ya kukusanya fasihi

      

Eleza udhaifu wa kushiriki kama njia ya kukusanya fasihi.

  

Answers


KELVIN
a) Huchukua muda mrefu kulingana na njia nyinginezo kama vile hojaji au mahojiano.
b) Mtafiti huweza kutekwa na yaliomo akasahau kurekodi.
c) Ugeni wa mtafiti huweza kuleta wasiwasi miongoni mwa washiriki wakakosa kufanya kama kawaida.
d) Uchanganuzi wa data ikusanywayo kwa njia hii ni ngumu, lakini rahisi kwa mtafiti kuacha maswala muhimu. Ni njia ghali ya utafiti kwani inamhitaji mtafiti kusafiri mbali ili kushiriki katika utendaji pia vifaa vya kuhifadhia data yenyewe kama vile kanda za video huwa ghali na nguvu za umeme huenda zikakosa.

kalvinspartan answered the question on August 5, 2018 at 12:43


Next: Eleza maana ya kushiriki kama njia mojawapo ya kukusanya fasihi huku ukitoa umuhimu wake
Previous: Fafanua kurekodi kama njia mojawapo ya kukusanya fasihi

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions