Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Eleza sababu ambazo zinafanya hojaji zisitumiwe kukusanya fasihi

      

Eleza sababu ambazo zinafanya hojaji zisitumiwe kukusanya fasihi.

  

Answers


KELVIN
a) Maswali yenye utata husababisha fasiri mbalimbali zifanyazo mategemeo yasitegemeke.
b) Huenda watu wakakosa kuijaza hojaji kwa kikamilifu kwa sababu mbalimbali kama vile kuhofia lawama au wakakataa kujaza kabisa.
c) Hojaji ndefu huenda baadhi ya watu wakakataa kuijaza.
d) Hojaji wazi huwa ngumu sana kwa mtafiti kuchanganua data, uchanganuzi huchukua muda mrefu.
e) Huenda wahojiwa wasijaze mambo ya kweli, si rahisi kwa mtafiti kuthibitisha kama habari zilizojazwa ni kweli.
f) Wahojiwa wanaweza kuchelewa kutuma hojaji zao, hasa zinazotumwa kwa posta.
g) Baadhi ya wazee, japo wana habari za kutegemewa, hawajui kusoma na kuandika hivyo hawawezi kujaza hojaji isipokuwa waanaposaidiwa na watafiti.
h) Kwa vile mtafiti hakabiliani na mhojiwa ana kwa ana, hawezi kupata sifa za uwasilishaji wa vipera vya fasihi simulizi kama vile toni na kidatu.

kalvinspartan answered the question on August 5, 2018 at 12:51


Next: Umuhimu wa hojaji zinapotumiwa kukusanya fasihi
Previous: Mahojiano ninjia mojawapo ya kukusanya kazi ya fasihi.eleza maana yake huku ukitolea umihumu wake

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions