Mahojiano ninjia mojawapo ya kukusanya kazi ya fasihi.eleza maana yake huku ukitolea umihumu wake

      

Mahojiano ninjia mojawapo ya kukusanya kazi ya fasihi.eleza maana yake huku ukitolea umihumu wake.

  

Answers


KELVIN
Mkusanyaji hakabiliana ana kwa ana na watu anaonuia kupata maarifa kutoka kwao. Mkusanyaji atakuwa ameandaa maswali atakayouliza katika kikao rasmi mkusanyaji pia anaweza kushiriki mahojiano yasiyo rasmi bila kunakili majibu papo hapo, maelezo huweza kuhifadhiwa katika kanda ya kunasa sauti.
Umuhimu wa mahojiano
a) Kwa vile mtafiti anatazama ana kwa ana na mhojiwa ni rahisi kupata habari za kina na kutegemeka.
b) Mbinu za uwasilishaji k.m toni, ishara za uso na kiimbo hubainika kwa mtafiti hivyo kuimarisha uelewa wake.
c) Mtafiti anaweza kumfafanulia mhojiwa maswali na kumwezesha kupata data ya kuaminika zaidi.
d) Kwa vile mtafiti anamhoji mlengwa moja kwa moja anaweza kurekodi majibu ya mhojiwa moja kwa moja au kuyaandika, si rahisi kupotea.
e) Mtafiti huweza kubadilisha mtindo wa kuhoji kulingana na kiwango cha elimu cha mhojiwa, ili kupata majibu bora zaidi.

kalvinspartan answered the question on August 5, 2018 at 12:52


Next: Eleza sababu ambazo zinafanya hojaji zisitumiwe kukusanya fasihi
Previous: Taja sababu ambazo wewe kama anayekusanya kazi ya fasihi zingechnagia kutotumia mahojiano

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions