Udhaifu unakabili matumizi ya kalamu na karatasi katika kuhifadhi data

      

Udhaifu unakabili matumizi ya kalamu na karatasi katika kuhifadhi data.

  

Answers


KELVIN
a) Kuna mambo k.m kiimbo, toni, ishara, hisia na mapigo ya mziki ambayo hayawezi kuandikwa kama yalivyowasilishwa na fanani, hivyo hupotea.
b) Aidha, kwa vile maandishi si hai, hayawezi kutenda wala kusema ule uhai hasilia wa fasihi simulizi hufifishwa na kupotezwa na maandishi
c) Baadhi ya watafiti huenda wakandika yale ambayo wanahitaji kwa wakati mahususi na kupuuza mengine k.m ikiwa mada yake ni ‘wahusika katika ngano za kimapokeo’ huenda akajihusisha na wahusika na kupuuza vipengele vingine k.m fanani haya huipunja fasihi simulizi
d) Kuandika fasihi simulizi huifanya kukosa ile taathira asilia kwani kunaipokonya hadhira yake ile fursa ya kushirikiana ana kwa ana na fanani, mtu hawezi kuuliza jambo
e) Kuandika fasihi simulizi huidhibiti na kupunguza hadhira yake na kuathiri vibaya usambazaji wake fasihi inapoandikwa inawafikia wale tu wanajua kusoma

kalvinspartan answered the question on August 5, 2018 at 12:57


Next: Eleza matumizi ya kalamu na karatasi katika kuhifadhi fasihi kisha utaje umihimu wake
Previous: Vinasasauti vinatumika kuhifadhi data ya fasihi kwa sababu gani

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions