Ukusanyaji na uhifadhi wa fasihi ni muhimu kwa sababu zipi

      

Ukusanyaji na uhifadhi wa fasihi ni muhimu kwa sababu zipi.

  

Answers


KELVIN
a) Fasihi simulizi ni hifadhi ya mitazamo ya kitamaduni ya jamii, ukusanyaji utampa mwanafunzi wa fasihi simulizi fursa ya kuingiliana na jamii iliyozaa fasihi husika ili kuweza kuielewa nyema.
b) Ukusanyaji humpa mwanafunzi wa fasihi simulizi nafasi ya kushuhudia na kuathiriwa moja kwa moja na utendaji wa fasihi simulizi hivyo mwanafunzi huona vipengele hai vya fasihi simulizi k.m uigizaji na hivyo kuielewa kwa kina.
c) Husaidia kurekodi na kuhifadhi tamaduni za jamii na kuzipitisha kwa vizazi vijavyo.
d) Ukusanyaji huiendeleza fasihi simulizi, kwa kurekodi vipera kama ngano, hekiya, historia na mtazamo wa kijumla wa jamii kuhusu maisha huhifadhiwa na kupitishwa
e) Husaidia kuziba pengo la utafiti lililopo, tanzu nyingi za fasihi simulizi hazijafanyiwa utafiti wa kutosha ili kuzihifadhi ukusanyaji utasaidia kuziba pengo hili.
f) Hutumika kama msingi wa uchunguzi wa kiulinganishi wa fasihi simulizi za jamii mbalimbali k.m muundo wa utambaji ngano katika jamii mbalimbali.
g) Ili kuelewa ni kwa nini kwa mfano, utungo mmoja wa fasihi simulizi ukawasilishwa kwa njia tofauti katika muktadha tofauti/jambo hili huwawezesha watafiti na wasomi kuelewa sifa za tungo za fasihi.
h) Utafiti wa fasihi simulizi huwezesha mwanafunzi kupata maarifa au stadi za kufanya utafiti katika taaluma nyingine k.m sosholojia.
i) Husaidia kurekebisha mawazo potovu kuhusu fasihi simulizi k.m kujua ni tanzu gani zilizokuwa za awali kabisa. Umewawezesha wasomi kutambua kuwa tungo nyingi zilizoandikwa zilitokana na simulizi za tungo za fasihi simulizi k.m riwaya, hadithi fupi na novella.

kalvinspartan answered the question on August 5, 2018 at 13:02


Next: Filamu zina changamoto kadhaa ambazo hutatiza matumizi yake kuhifadhi fasihi
Previous: Nini maana ya silabi?

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions