Huku ukitolea mifano, eleza aina tofauti za nomino

      

Huku ukitolea mifano, eleza aina tofauti za nomino

  

Answers


KELVIN
? Neno linalotaja kiumbe, kitu, hali, mahali, tendo, dhana, n.k.
Aina
? Nomino za Pekee
? Ambazo hutaja kitu kwa kutumia jina lake/ambazo hutambulisha upekee wa kitu hicho.
? Mwanzoni huandikwa kwa herufi kubwa.
? majina ya watu k.m. Kamau
? mahali k.m. Mombasa
? siku k.m. Alhamisi
? miezi k.m. Disemba
? miaka k.m. 1930
? milima k.m. Kilimanjaro
? Mito k.m. Tana
? maziwa k.m. Victoria
? bahari k.m. Hindi
? Mabara k.m. Africa

? Nomono za Kawaida/Jumla
? Majina ya jumla ya viumbe/vitu vinavyoonyesha umbile la jinsi moja k.m. mtu, gari, kalamu, n.k.
? Nomino za Jamii
? Majina ya makundi ya viumbe au vitu k.m. bunge, jamii, halaiki, bunda n.k.
? Nomino za Wingi
? Majina ya vitu vitokeavyo kwa wingi japo kimsingi hazina umoja au wingi k.m. maji, mate, maziwa, mahubiri, marashi, mchanga, ngeu, poda, unga, n.k.
? Nomino za Dhahania
? Majina ya viumbe au mambo ya kudhani/yasiyoweza kugusika k.m. k.m ujinga, werevu, malaika, shetani, amani, imani, roho, wazo, dhana, n.k.
? Nomino za Vitenzi Jina
? Vitenzi vyenye kiambishi awali ku ambavyo huweza pia kutumika kama nomino k.m. Kucheza kwake kunaudhi.

kalvinspartan answered the question on August 5, 2018 at 13:18


Next: Viyeyusho au nusu irabu ni sauti gani?
Previous: Eleza maana ya sentensi katika kiswahili huku ukitoa sifa zake

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions