? Nomino kutokana na mzizi wa kitenzi
a) danganya-kudanganya, mdanganyifu,udanganyifu
b) soma-kusoma, masomo,msomi,usomaji
c) unda-kuunda, muundaji,uundaji,muundo
d) funika-kufunika, kifuniko, mfunikaji, ufunikaji
? Kitenzi kutokana na mzizi wa nomino
a) mlo-kula
b) mlevi-kulewa, kulevuka
c) mwimbaji-kuimba
d) fikra-kufikiri
e) malezi-kulea
f) fumbo-kufumba, kufumbua
? Nomino kutokana na mzizi wa nomino
a) mwimbaji-kuimba, wimbo, uimbaji, kiimbo
b) mchezo-kucheza, uchezaji, mchezaji
c) ulaghai-kulaghai, mlaghai
d) hesabu-kuhesabu,uhesabu
e) mdhalimu- kudhulumu, dhuluma, udhalimu
? Nomino kutokana na mzizi wa kivumishi
a) -refu-mrefu, urefu, urefushaji
b) -baya-mbaya, ubaya
c) -zuri-mzuri, uzuri
d) -kali-mkali, ukali
e) -eupe-mweupe,weupe
? Kivumishi kutokana na mzizi wa nomino
a) ujinga -jinga
b) werevu -erevu
c) mzuri -zuri
d) mpumbavu -pumbavu
e) mpyoro -pyoro
? Kitenzi kutokana na mzizi wa kivumishi
a) haramu-kuharamisha, kuharamika
b) halali-kuhalalisha, kuhalalika
c) -fupi-kufupisha, kufupika
d) bora-kuboresha, kuboreka
e) -refu-kurefusha, kurefuka
f) sahihi-kusahihisha, kusahihika
g) -sikivu-kusikia
h) -danganyifu-kudanganya
? Kivumishi kutokana na mzizi wa kitenzi
a) dunisha - duni
b) Haramisha - haramu
c) fupisha -fupi
d) sahilisha -sahili
e) tukuka -tukufu
f) fahamu -fahamivu
g) teua -teule
h) nyamaza -nyamavu
i) ongoka -ongofu
j) sahihisha -sahihi
k) danganya -danganyifu
? Kitenzi kutokana na kielezi
a) haraka-harakisha
b) zaidi-zidisha
c) bidii-bidiisha
d) hima-himiza
kalvinspartan answered the question on August 10, 2018 at 08:16