Tambua na ueleze aina tofauti za vielezi

      

Tambua na ueleze aina tofauti za vielezi.

  

Answers


KELVIN
a) Vielezi vya Namna/Jinsi
? Ambavyo hueleza vile jambo lilifanyika.
Aina
? Vielezi namna mfanano
? Vinavyoeleza vile jambo lilifanyika kwa kufananisha na nomino au vivumishi.
? Huchukua viambishi KI na VI.
? Anakula kifisi.
? Tulifanya kazi vizuri.
? Vielezi namna viigizi
? Maneno ambayo kiasili ni vielezi k.m. sana, haraka, ghafla, mno, kabisa, pole, barabara n.k.
? Mwenda pole hajikwai.
? Vielezi namna hali
? Hueleza hali ya tendo.
? Alilelewa kwa shida.
? Alilewa chakari
? Vielezi namna vikariri
? Huelezea vile jambo lilifanyika kwa kurudiwarudiwa
? Alinijibu kimzahamzaha.
? Tembea polepole.
? Yeye hufanya kazi yake hivi hivi/ovyo ovyo
? Mbwa alibweka bwe! Bwe! Bwe!
? Vielezi namna ala
? Walimpiga Stephano mawe/kwa mawe.
? Vielezi Namna Viigizi
? Hueleza vile kitendo kilitendeka kwa kutumia tanakali.
? Mbuni alianguka majini chubwi!
b) Vielezi vya Idadi/Kiasi
? Maneno ambayo hutaja kitendo kimetendeka mara ngapi.
Aina
? Vielezi vya idadi halisi
? Tulivamiwa mara moja.
? Vielezi vya idadi ya jumla
? Alitoroka mara kadha/nyingi/chache.
c) Vielezi vya mahali
? Hutaja mahali kitendo kilitendekea.
Aina
? Vielezi vya mahali vya maneno kamili
? Ndege ilipofika Nairobi, ilitua chini.
? Vielezi vya mahali vya aina ya viambishi
? Ni viambishi po, ko, mo na ni.
? Alipolala palikuwa na siafu.
? Wanacheza uwanjani.
d) Vielezi vya wakati
? Hutaja kitendo kililifanyika wakati gani.
Aina
? Vielezi vya wakati vya maneno kamili
? Rais atawasili kesho/mwaka ujao.
? Kielezi cha wakati cha kiambishi (po ya wakati)
? Nililala nilipofika nyumbani

kalvinspartan answered the question on August 10, 2018 at 08:29


Next: Jadili vielezi
Previous: Jadili viunganishi

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions