Kwa kudhidirisha katika sentensi onyesha jinsi aina tofauti za maneno huingiliana

      

Kwa kudhidirisha katika sentensi onyesha jinsi aina tofauti za maneno huingiliana.

  

Answers


KELVIN
? Hali ya maneno kuwa na matumizi tofauti mifano:

? W kuwa V
? Huyu analia.
? Mtoto huyu analia.
? V kuwa W
? Vikombe vizuri vitavunjika.
? Vizuri vitaliwa.
? V kuwa N
? Mti mrefu haupandiki.
? Mrefu alikufa jana jioni.
? V kuwa E
? Viatu vibaya vitachomwa.
? Uliifanya kazi vibaya.
? Mtu mjinga ni huyu.
? Anaongea kijinga.
? N kuwa V
? Tajiri alimdharau Razaro.
? Mtu tajiri huheshimiwa.
? N kuwa E
? Nairobi ni mji mkuu.
? Amewasili Nairobi.
? Kitoto kinalia.
? Unaongea kitoto.
? Haraka haina baraka.
? Fanya haraka tuondoke hapa.
? Sindano ya babu imepotea
? Alidungwa sindano/kwa sindano na daktari.
? E kuwa N
? Niliwasili jana.
? Jana yangu haikuwa nzuri.
? T kuwa N
? Nataka kulala sasa.
? Kulala kwake kunaudhi.
? N kuwa U
? Ila yake imemwathiri sana.
? Watu wote ila yeye walikwenda.
? Kichwa changu kina walakini.
? Nimekula walakini sijashiba.
? E kuwa I
? Mwenda pole hajikwai.
? Pole! Usijali utapona.
? Amepaka rangi sawasawa.
? Sawasawa! Siku moja tutakutana.
? H kuwa E
? Paka amepanda juu ya mti.
? Ameingia katika choo.
? T kuwa E
? Mtoto akilia atatapika.
? Aliingia akilia.
? N kuwa I
? Gege anacheza ala yake ya muziki.
? Ala! Waniwekea uchafu katika chakula?



kalvinspartan answered the question on August 10, 2018 at 08:36


Next: Eleza maana ya vihisishi huku ukieleza aina tofauti
Previous: Eleza maana mofimu

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions