Jadili kauli mbali mbali ambazo kitenzi hunyambuliwa

      

Jadili kauli mbali mbali ambazo kitenzi hunyambuliwa.

  

Answers


KELVIN
? Kutenda
? Hali ya kawaida ya kitenzi.
? Kutendatenda
? Hali ya kitenzi kurudiwa.
? Kutendea
? Kwa niaba ya
? Badala ya
? Sababu
? Kuonyesha kitumizi
? Mwendo wa kitu kuelekea kingine
? Kutendwa
? Huonyesha nomino iliyoathiriwa na kitenzi.
? Kutendewa
? Humaanisha kitendo kimetendwa na mtu badala au kwa niaba ya mtu mwingine.
? Kutendana
? Unamtenda mtu jambo naye anakutenda jambo lilo hilo.
? Kutendeana
? Unamtendea mtu jambo naye anakutendea jambo lilo hilo.
? Kutendeka
? Uwezekano wa kitendo kufanyika
? Kutendesha
? Mtu au kitu kusababisha kufanyika kwa kitendo.
? Kutendeshea
? Kusababisha kitendo kitendeke kwa niaba ya mwingine.
? Kutendeshwa
? Kusababishwa kufanya jambo.
? Kutendeshewa
? Mtu kusababishwa kitendo kitendeke kwa niaba yake.
? Kutendeshana
? Kusababisha kitendo kitendeke kwa mtu naye anasababisha kitendo kicho hicho kitendeke kwako.
? Kutendesheana
? Kusababisha kitendo kitendeke kwa niaba ya mtu naye anasababisha kitendo kicho hicho kitendeke kwa niaba yako.
? Kutendesheka
? Kitendo fulani kinaweza kusaababishwa.
? Kutendama
? Kuwa katika hali fulani bila ya mabadiliko.
? lala-lalama
? ficha-fichama
? shika-shikama
? ganda-gandama
? chuta-chutama
? funga-fungama
? kwaa-kwama
? unga-ungama
? andaa-andama
? saki-sakama
? Kutendata
? Hali ya mgusano au kushikanisha vitu viwili.

? paka-pakata
? fumba-fumbata
? kokoa-kokota
? okoa-okota
? kama-kamata

? Kutendua
? Hali ya kiyume

? choma-chomoa
? funga-fungua
? Kutenduka
? Kuweza kufanyika kwa hali ya kinyume.

? chomoka
? funguka
kalvinspartan answered the question on August 10, 2018 at 08:41


Next: Jadili aina tofauti za viambishi
Previous: Eleza kwa kutolea mifano matumizi ya neno ila

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions