Onyesha matumizi ya kwa

      

onyesha matumizi ya kwa

  

Answers


KELVIN
a) mahali
? Ameenda kwa Juma.
b) jinsi
? Alisoma kwa bidii.
c) sehemu ya kitu kisima/akisami
? Amepata alama moja kwa tano katika mtihani.
d) pamoja na
? Harusi ilihudhuliwa na wazee kwa vijana na tulikula wali kwa nyama.
e) kuonyesha kitu kilitumiwa kama kifaa
? Alikata mkate kwa kisu.
f) sababu
? Aliugua kwa kunywa maji machafu.
g) kuunganisha vipashio viwili
? Leo ndiwe utapika kwa hivyo tayarisha viazi.
h) muda/kipindi
? Alilia kwa nusu sana.
i) kufanya jambo bila kupoteza wakati
? Baada ya kula, tulienda moja kwa moja kulala.
j) kivumishi cha a-unganifu cha ngeli ya KU
? Kucheka kwa Maria kunaudhi.
k) umiliki wa mahali
? Twende nyumbani kwangu.

kalvinspartan answered the question on August 10, 2018 at 08:58


Next: Onyesha matumizi tofauti ya jinsi
Previous: Onyesha matumizi tofauti ya na

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions